Usajili wa vikosi vitakovyo wakilisha timu shiriki katika ligi kuu Tanzania bara 2011/12 utafunguliwa rasmi hapo juni 2 mwaka huu.
Vilabu shiriki vinaendelea kusaka nyota na kuwapa mikataba baadhi yao, huku wakingoja muda uliopangwa wa usajili kukamilisha usajili wao.
Katibu mkuu wa chama cha wachezaji Said George amewataka wachezaji wawe makini katika mikataba wanayo ingia na vilabu.
George alisema wanataka kuwepo kwa utaratibu maalum kuhusu mikataba hiyo, kwani mara nyingi hata klabu hazitimizi wajibu wao kwa wachezaji wao na hata soka la kulipwa kama linavyozungumzwa bado halipo nchini.
TFF KUBADILI MFUMO WA LIGI.
Tff wanataka kubadili mfumo wa ligi kutoka kuwa chini ya Tff kwenda kwa kambuni ambayo itakuwa inasimamia ligi hiyo.
Kwa hali hiyo Tff wameiomba fifa iwatumie mtaalam atakaye wasaidia katika hilo na mambo ya kienda sawa mfumo huo mpya utaanza kutumika katika ligi ya msimu wa 2011/12.
TFF wamefikia uwamuzi huo, ili washughulike vyema katika maendeleo ya soka nchini. Kwa taratibu hiyo mpya ligi zake kuanzia ligi kuu ya vodacom, ligi daraja la kwanza na ligi ngazi ya taifa zitasimamiwa na kampuni wakisaidiana na vilabu husika.
aamsuni
0 comments:
Post a Comment