VPL

Ruvu Shooting timu yenye nidhamu, Masawe mchezaji bora

Kampuni ya simu ya vodacom leo walitoa fedha kwa timu, wachezaji, kocha na mwamuzi waliofanya vyema katika ligi kuu ya vodacom (VPL) msimu wa 2010/2011 katika hafla ya chakula cha mchana iliyo andaliwa na TFF wakishirikiana na Vodacom.

MWAMUZI BORA.
Mwamuzi toka mkoani mwanza Alex Mahajiwa amefanikiwa kuwa mwamuzi bora katika msimu wa 2010/11 na kujizolea kitita cha tsh milioni 3.1.

KOCHA BORA.
Kocha aliyemaliza mkataba katika klabu ya Simba, mzambia Patrick Phiri amefanikiwa tena kutwaa tuzo ya Kocha bora mara ya pili mfululizo.
Phiri alitwaa tuzo hiyo msimu wa 2009/10 kwa kuiwezesha Simba kutwa ubingwa bila ya kufungwa na katika msimu wa 2010/11 aliiwezesha Simba kuongoza ligi kwa takribani mzunguko wote wa pili na mwisho wa siku kujikuta wanakamata nafasi ya pili. Phiri atakabithiwa tsh milion 3.1.

MCHEZAJI BORA.
Jacob Massawe anae cheza katika klabu ya Toto African ya Mwanza ametangazwa kuwa mchezaji bora wa msimu akimpiku Mrisho Ngassa aliyechukuwa msimu wa 2009/10 akiwa Yanga.
Massawe amepokea hundi ya tsh milion 2.65.

KIPA BORA.
Tuzo ya kipa bora imeenda kwa mlinda mlango wa Yanga Yaw Berko baada ya kuiwezesha yanga kutwa ubingwa huku nyavu zake zikitingishwa mara chache kuliko makipa wengine. Berko ameondoka na hundi ya tsh milion 2.65

MFUNGAJI BORA.
Mshambuliaji wa Azam fc Mrisho Khalfan Ngassa ameibuka mfungaji bora baada ya kutikisa nyavu mara 15 akimbwaga Gaudence Mwaikimba (kagera sugar) na John Boko (azam fc). Ngassa meondoka na kitita cha tsh milion 3.1

TIMU YENYE NIDHAMU.
Timu ya Ruvu Shooting ya Pwani imetwa tuzo ya timu yenye nidhamu baada ya kuibwaga yanga ambayo ndio timu iliyopewa kadi chache lakini kwa matukio mawili waliyo yafanya katika mechi zake ikiwa na lile la kufanya uaribifu katika uwanja wa Majimaji na vurugu katika uwanja wa jamhuri morogoro walipo ikaribisha Kagera Sugari.
Ruvu shooting imezawadiwa tsh milioni 6.2.

TATU BORA.
Timu ya Azam fc imechukua kiasi cha tsh milion 11 kwa kusika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi.
Timu ya Simba sc imechukua kiasi cha tsh milioni 17, kwa kushika nafasi ya pili.
Bingwa wa ligi hiyo, Yanga walipewa hundi ya sh milioni 42.


aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.