Timu ya soka ya Simba leo inateremka katika uwanja wa petrosport jijini Cairo kuwavaa wa Wydad Casabalance katika mchezo wa kusaka timu itakayo ingia katika nane bora ya klabu bingwa Africa, badala ya TP Mazembe ambayo ilivuliwa ubingwa na CAF baada ya Rufaa ya Simba kupitishwa.
JIJI LA CAIRO.
Jiji la Cairo kama majiji mengini ya nchi za kiarabu imekuwa ngumu kwa timu za Africa kutoka na ushindi pale wanapo kabiliana na timu za kiarabu. Timu ngeni hukutani kila aina ya fitna za nnje ya uwanja.Simba mara ya mwisho kwenda Misri walifungwa goli tano kwa mbili katika mchezo wa Shirikisho hapo mwaka jana. Kabla ya kupokea kichapo hicho Simba waliisambaratisha timu ya Zamaleki katika mchezo wa raundi ya mwisho wa klabu bingwa Africa mwaka 2003 na kutinga nane bora kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu ya Simba.
JUMA K JUMA.
Juma Kaseja 'Cassilas wa bongo' alipata umaarufu mkubwa barani Afrika baada ya mchezo na Zamalek ambapo alionyesha kiwango kikubwa katika mchezo huo kwa kucheza vyema mpira ya krosi mashuti ya waarabu na mwisho kabisa kuokoa michomo ya penati.
Kaseja ndie mchezaji pekee aliyesalia katika kikosi kilicho iangamiza Zameleki jijini Cairo na leo ataiongoza simba katika kuweka maajabu pale watakapo wakabili Wydad.
Pamoja na kuaminiwa kwake Kaseja na kuwa nguzo muhimu kwa Simba katika kipindi chote alicho kitumikia Simba, hivi sasa anaonekana akifungwa magoli ambayo ilikuwa ngumu kumfunga kipindi cha nyuma hususani baada ya kupokea goli 5 mapema mwaka huu katika mashindano ya mto nile yaliyo fanyika jijini Cairo.
Mashabiki wa Simba wanamatumaini na Juma Kaseja leo kuliongoza jaazi la Simba na kurejesha makali yake yaliyo potelea Cairo.
KIKOSI CHA SIMBA.
Kikosi kilicho jifua kwa wiki moja chini ya kocha Basena kina kazi kubwa mbele yake kuweka historia mpya klabuni hapo. Kikosi hicho kinaundwa na wachezaji walio tuhumiwa kuhujumu timu, wanakabiliana na timu ambayo bado iko mashindanoni ukilinganisha na simba ambapo walikuwa kwenye likizo ambayo imekatishwa ghafla wakati wengine wakiwa katika mihangaiko ya kusaka timu watakazo zitumikia msimu ujao.
Kocha Basena ambaye kakaa na timu mda mfupi na mechi ya leo ni mechi yake ya kwanza anaimani na kikosi chake na amejinasibu wanaenda kuonyesha maajabu ya soka.
Pamoja na hayo yote simba wanao nafasi ya kushinda leo pamoja na kuwa kosa mshambuliaji Mbwana Samata na Ochan, kama wataweka tofauti zao pembeni na kucheza kwa hari bila shaka wataweka historia mpya hii leo.
Kikosi kinacho weza kuanza leo ni:
1. JUMA K JUMA
2. HARUNA SHAMTE
3. AMIR MAFTAH
4. KELVIN YONDANI
5. JUMA NYOSO
6. JERRY SANTO
7. NICO NYAGAWA
8. ECHESA
9. MUSSA MGOSI
10. EMANUEL OKWI
11. AMIR KIEMBA
MUNGU IBARIKI SIMBA MUNGU IBARIKI TANZANIA
aamsuni

0 comments:
Post a Comment