Timu ya Simba leo imeshindwa kutamba katika mchezo wa klabu bingwa Afrika nchini Misri baada ya kukubali kichapo cha goli tatu kwa bila toka kwa Wydad Casabalance.
Simba waliuwanza mchezo kwa kujihami zaidi na kufanikiwa kwenda mapumziko bila kufungana.
Kipindi cha pili Wydad waliendelea kulisakama goli la Simba bila mafanikio huku kukiwepo na kosa kosa nyingi golini mwa simba.
Wakati mashabiki wakingoja kuona dakika 30 za nyongeza kisha matuta, mambo yaliwaendea kombo Simba na kujikuta wanaruhusu magoli matatu ya haraka katika dakika za 88, 89 na 91 mpira kwisha.
Kwa matokeo hayo Wydad anaenda kuungana na Waarabu wenzake katika kundi B ambalo lina timu za Al ahly (Misri), Esperance (Tunisia) na Moloudia Club d' Alger (Algeria).
Wakati mnyama Simba ameangukia kwenye kombe la shirikisho hatua ya 16 bora na itapambana na timu ya Daring Club Motema Pembe ya DRC kati ya Juni10 , 11 na 12 mwaka huu.
aamsuni

0 comments:
Post a Comment