Timu ya simba ambayo ilishinda rufaa yake wamejikuta wakiwa na waarabu. Simba imepangwa kundi B zenye timu kutoka Algeria, Tunisia na Misri endapo watamfunga Wydad Casablanca ya Moroco.
Simba watacheza na Wydad Casablanca mwishoni mwa juma kutafuta timu itakayo chukua nafasi ya TP Mazembe ambayo ilikuwa teyari isha fuzu kwa hatua ya nane bora kabla ya kuvuliwa ubingwa kwa rufaa ya Simba.
Simba wanatarajiwa kuanza kutafuta makali leo ya kuinyonga Wydada. "Kesho(leo) tunaanza mazoezi, jambo muhimu naomba uongozi uwaite haraka, hii ni fursa ya aina yake tunatakiwa tujipange ili tuweze kupambana na kupata matokeo mazuri," alisema kocha wa simba Basena.
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu alisema, simba watatumia nyota wake waliouzwa katika pambano na Wydada kwa kuwa bado ITC zao hazija tumwa. “Simba itawatumia wachezaji wake waliosajiliwa kushiriki mashindano ya klabu bingwa wakiwemo wale waliouzwa TP Mazembe, wachezaji hao bado ni mali ya Simba ingawa wameshauzwa, lakini uhalali wa mchezaji kuuzwa ni ITC na mpaka hivi sasa TP Mazembe haijaomba ITC ya wachezaji hao, hivyo bado wanahesabika kama wachezaji halali wa Simba katika mashindano haya,” alisema Kaburu.
Makundi ya klabu bingwa Africa yaliyotangazwa hapo jana:
Kundi A;
Hilal (Sudan)
Coton Sport Garoua (Cameroon)
Enyimba (Nigeria)
Raja (Morocco)
Kundi B;
Ahly (Misri)
EST (Tunisia)
Moloudia Club d’Alger (Algeria)
Simba (Tanzania) au Widad de Casablanca (Morocco)
aamsuni

0 comments:
Post a Comment