Bingwa mtetezi wa Kili Taifa Cup imevuliwa ubingwa rasmi hii leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid baada ya kulala magoli 3.
Timu ya mkoa wa Singida ambaye ndiye bingwa wa kili taifa cup 2010, ilikubali kulala goli 3 bila majibu toka kwa watoto wa mjini timu ya mkoa wa Ilala, katika mchezo wa awali wa robo fainali.
Katika mpambano mwingine wa robo fainali uliwakutanisha mwenyeji, Arusha na timu ya mkoa wa Mwanza. Katika pambano hilo timu ya Mwanza iliibuka kidedea kwa kuichalaza Arusha magoli mawili kwa moja.
Kutokana na matokeo hayo nusu fainali ya Kwanza itakayo chezwa mei 24 itawakutanisha timu ya Mwanza na Ilala.
Kesho michuano ya kili taifa cup 2011 itaendelea kwa michezo miwili ya robo fainali katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Mchezo wa kwanza itakuwa baina ya Ruvuma na Mbeya utakao anza saa nane na kufuatiwa na mchezo baina ya Kagera na timu ya taifa chini ya miaka 23.
Washindi wa michezo hiyo miwili ndio watakao kutana katika nusu fainali ya pili itakayochezwa mei 25 huku fainali ikipigwa mei 28.
aamsuni

0 comments:
Post a Comment