Timu iliyorejea ligi kuu yenye maskani yake Tabata jijini Dar es salaam, Moro United imesema wanatarajia kuunda kikosi B kutoka katika mashindano ya street cup.
Mashindano hayo ya street cup ambayo huchezwa siku za wikiend katika viwanja vya shule ya msingi ya Tabata huusisha vijana chini ya miaka 20. Moro united imeweka dhamira hiyo huku wakiendelea kuyafuatilia michuano hiyo kwa ajili ya timu B.
MTIBWA SUGAR: FUATENI KANUNI.
Uongozi wa mtibwa sugar umesema kwa zile timu wanao waitaji wachezaji wake wenye mkataba wanatakiwa kufuata taratibu ili kuepusha migogoro hapo baadae.
Kauli hiyo inakuja baada ya kuripotiwa kipa mahiri wa timu hiyo pamoja na timu ya taifa, Shabani Kado kusaini yanga mkataba wa miaka miwili huku akiwa na mkataba na mtibwa sugar.
Uongozi huo unasema kuwa alikuja mtu wa yanga katika mazungumzo akaingizia suala la Kado na wao kumpatia masharti yao lakini hakurudi tena na wala alipokuja hakuja kwa suala ilo kwakuwa hakuwa na baruwa.
Nnje ya Kado wachezaji wengine walio ondoka mtibwa sugar ni Julias Mrope (Yanga), Salum Machaku (Simba), Yona Ndambila (Klabu ya China), Salum Swedi (Klabu ya Msumbiji).
WAGHANA WAWILI KUTUA AZAM FC.
Usajili wa Azam fc utafungwa pale wachezaji toka Ghana watakapo wasili nchini hapo juni 7 pamoja na Muivorcoast Kipre. Waghana hao wamechelewa kutokana na kubanwa na ligi ya nchini humo ambayo itafikia tamati juni 5.
Katika hatua nyingine kocha wa Azam Hall anatarajiwa kurejea nchini hapo juni 5 kwa ajili ya maandalizi yatakayoanza juni 10.
KAGERA SUGAR KURUDISHA MATAPISHI YAO.
Timu ya Kagera sugar wako mbioni kumrejesha beki Maligesi Mangwa baada ya kufanya vyema katika kombe la Taifa cup ambapo aliiwakilisha timu ya mkoa wa Mwanza.
Maligesi anachukuliwa na Kagera baada ya safu yake ya ulinzi kubomolewa na Azam fc pamoja na Yanga.
Katika hatua nyingine timu hiyo xa wakatamiwa wanatarajia kusajili nyota wa tano walio fanya vyema katika kombe la taifa cup lililo malizika majuzi kwa mbeya kutwaa ubingwa.
Wakata miwa hao wamesema Mwaikimba msimu ujao ataitumikia klabu hiyo kwakuwa bado wana muhitaji.
SAMATA LULU TIMU ZA TAIFA.
Mshambuliaji wa TP Mazembe Mbwana Samata amekuwa lulu katika timu za taifa baada ya Julio kuwa mgumu kukubali aitumikie Taifa stars wakati naye Poulsen akimuihitaji.
USAJILI WA LIGI KUU YA VODACOM UNATARAJIWA KUFUNGULIWA JUNI 20 MPAKA JULAI 20 HUKU KLABU ZA SIMBA, YANGA NA AZAM WAKIWA WAMESHA KAMILISHA KWA KIWANGO KIKUBWA, HUKU TIMU NYINGINE BADO ZIKIWA KATIKA MAWINDO.
aamsuni
source: mwanaspot na majira

0 comments:
Post a Comment