Vifaa kwa ajili ya maandilizi ya michuano ya vijana chini ya miaka 17, copa coca cola vimeanza kutolewa kwa timu shiriki.
Michuano hiyo ambayo hufanyika kila mwaka, inatarajiwa kuanza juni 11 katika vituo vya Dar es salaam na Kibaha.
Afisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema, timu zilizopo Dar es salaam (mikoa ya kisoka Ilala, Temeke na Kinondoni) watapokea vifaa vyao katika ofisi za Tff, wakati timu za mikoani mawasiliano yanaendelea ili kujua vifaa pamoja na fedha vitawafikiaje, huku akizitaka timu zilizoko jirani kuzifuata.
"Zile fedha kwa ajili ya maandalizi
ya ngazi ya wilaya ambazo
zilichelewa kufika zimefika kwa
hiyo wakichukua vifaa na fedha
za maandalizi ya mashindano
hayo ngazi ya taifa watapewa
pamoja na zile ambazo
zilichelewa"alisema Wambura.
aamsuni
0 comments:
Post a Comment