Watoto wa jiji 'rock city', Mwanza wamefanikiwa kuondoka na ushindi mbele ya watoto wa mjini 'city center', Ilala katika mchezo wa nusu fainali ya kili taifa cup.
Mwanza wamechungulia nyavu za Ilala mara mbili na zote hizo, zikichunguliwa na Jerry Tegete wakati vijana wa Ilala wakichungulia mara moja.
Jerry Tegete amefikisha magoli sita katika mashindano haya ya kili taifa cup ambapo mfungaji bora anaondoka na kitita cha tsh mili 2.5. Tegete anafukuzana na mshambuliaji wa jiji la Mbeya Gaudence Mwaikimba.
Kwa matokeo hayo timu ya Mwanza inayonolewa na kocha Tegete imetinga fainali na inangoja mshindi wa mechi ya kesho kwa ajili ya fainali itakayo chezwa mei 28. Wakati Ilala wakisaka nafasi ya mshindi wa tatu hapo mei 27.
MBEYA KINYWANI MWA KAGERA.
Timu ya mkoa wa Mbeya inayoongozwa na mshambuliaji wa Kagera sugar Gaudence Mwaikimba watakwaana na timu ya mko wa kagera katika nusu fainali ya pili itakayo chezwa hapo kesho katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Kagera ametokea katika kituo cha Mwanza kama best loser na kuiondoa mashindanoni timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 kwa mikwaju wa penati katika hatua ya robo fainali.
Mbeya aliibuka kinara wa kituo cha Mbeya na kisha kusambaratisha timu ya Ruvuma katika hatua ya robo fainali.
aamsuni
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment