VPL

Yanga kupokea hundi yao kesho

Kampuni ya simu ya Vodacom pamoja na Tff wameanda hafla ya chakula cha mchana kitakacho fanyika katika hotel ya Paradize kwa dhumuni ya kukabidhi hundi kwa washindi wa Vodacom premier league (VPL) 2010/11.
Katika hafla hiyo ambayo Dk Emanuel Nchimbi mwenye dhamana ya michezo atakuwa mgeni rasmi, huku timu za Yanga, Simba na Azam wakipokea hundi zao.

Vilevile kutakuwa na zawadi ya mfungaji bora ambaye alikuwa Mrisho khalfani Ngassa (Azam fc), kipa bora anaweza akawa Berko (Yanga), mwamuzi bora na
kocha bora.
Timu yenye nidhamu nayo itapokea zawadi hapo kesho na huenda ikawa Yanga ya jijini Dar es salaam.

Meneja udhamini na matukio Vodacom Tanzania, Rukia Mtigwa amesema wanafuraha kuona ligi inakwenda vyema huku zawadi zikitolewa kuamsha ushindani kwenye ligi. "Nifuraha kubwa kwetu tunapoona mambo yanakwenda vizuri kwani lengo la vodacom Tanzania ni kuona soka ikipiga hatua zaidi na hiyo ni pamoja na kuwa na ligi yenye zawadi zinazochochea ushindani na kesho bingwa yanga atakuwa na wakati mwingine wa kufurahia kazi waliyoifanya wakati wa ligi hadi kuibuka mabingwa," alisema Rukia.
Rukia aliendelea kufafanua ya kwamba zawadi za msimu wa 2010/11 zimeboreshwa ukilinganisha na zile za mwaka 2009/10. "Simba na Azam fc nao pia kesho tutawakabidhi hundi yao, pia wachezaji na wadau wengine waliongara kwenye msimu huo wa 2010/11 nao watakabidhiwa hundi zao zikiwa na nyongeza ikilinganishwa na zawadi za msimu wa 2009/10" alisema Rukia.


aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.