vilabu

Yanga watuma maombi tena

Uongozi wa klabu ya yanga wametuma barua ya maombi ya kumsajili Mrisho Khalfan Ngassa kwa klabu ya Azam fc hapo jana.
Nchunga akizungumza na waandishi wa habari hapo jana mda mchache baada ya uongozi wa Azam kuwataka wafuate taratibu kama wanamuhitaji mshambuliaji huyo. Alisema kuwa Yanga wanamuhitaji Ngasa na tayari wameshatuma barua yenye ofa ya Tsh mil 50 mchana huo. Ngassa aliuzwa kwa Azam FC akitokea yanga msimu uliopita kwa dau la Tsh mil 58.
Nchunga alilizungumzi suala la mshambuliaji Keneth Asamoh kutoka Ghana na kueleza kuwa bado hajasajiliwa na Yanga isipokuwa kuna majadiliano bado yanaendelea.
Nchunga alimalizia kwa kusema maandalizi ya tamasha la kumpongeza mfadhili wa Yanga, Yusuph Manji yanaendelea vyema na litafanyika kesho katika ukumbi wa PTA Uwanja wa Maonesho wa Sabasaba, jijini Dar es Salaam na itapabwa na bendi ya Msondo Ngoma pamoja na Sikinde ambazo zitatoa burudani siku hiyo.


aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.