Mchangani

Yusuph akabithiwa unaodha

 wachezaji watanzani wakimsikiliza kapteni
wachezaji wa Tanzamia wakimsikiliza 
kocha mpya baada ya uteuzi
Wachezaji wa timu ya Masai 'wanafunzi ambao hawajaanza facult', Yussuph na Adam wameteuliwa kuwa makapteni wa timu ya Tanzania ya wanafunzi wanao soma IUA nchini Sudan.

Kabla ya uteuzi huo kulikuwa na mchezo baina ya watanzania walioanza facult 'Wakongwe' na wale ambao hawajaanza 'wamasai', mchezo uliochezeshwa na Tego.
Katika mchezo huo uliochezwa katika kiwanja kidogo huku maguli yakiwa madogo ulimalizika kwa sare ya bila kufungana. Huku kukishuhudia wachezaji ambao walikuwa wametangaza kuachana na mpira wakionyesha uwezo wao akiwemo mwenyekiti mpya wa umoja wa wanafunzi wa Tanzania (TASU), Hadji akionesha uwezo wake.

Baada ya mchezo kuisha Katibu wa michezo na utamaduni, Mbarouk aliupongeza uwongozi ulio maliza muda wake hapo aprili mwaka huu, uliokuwa unaongozwa na Mugisha Katura akisaidiana na manahodha Baruwani na Omary Mbonde.
Alipeleka shukran maalumu kwa mchezaji Tumbo kwa moyo alio uonyesha katika kipindi cha Mugisha na baada ya Mugisha kumaliza mda wake.

Baada ya shukrani hizo aliendesha uteuzi wa makocha na makapteni wa timu ya Tanzania. Katika uteuzi huo, uliwapa uwanadhifa wa ukocha mkuu Tego huku akisaidiwa na Sadiki na upande wa makapteni aliteuliwa Yussuph kama kapteni akisaidiwa na Adam.

Tanzania wanatarajiwa kucheza mechi yao ya kwanza chini ya ungozi huo wa makapteni wiki baada ya wiki ijayo na timu ya Mali.

aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.