TFF

Safari ya Taifa stars yaota mbawa

Safari ya Taifa stars kwenda Sudan imeota mbawa baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan kufunjwa na kupelekea kambi ya Stars nayo kuvunjwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa TFF Boniface Wambura inasema, "Chama cha Mpira wa Miguu Sudan (SFA) kimefuta mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na timu ya Taifa ya nchi hiyo ‘Nile Crododile’ iliyokuwa ichezwe Agosti 10 mwaka huu. Uamuzi huo umetokana na wakala wa mechi hiyo Hadi Sharkawy kushindwa kupata kwa wakati tiketi ya kuisafirsha Taifa Stars kwenda Khartoum."

"Pia kutokana na mechi hiyo kufutwa, kambi ya Stars iliyokuwa hapa Dar es Salaam nayo imevunjwa leo." taarifa hiyo inaeleeza

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.