kitaa

Waandishi wa mchezo na wamiliki wa magazeti mpo

Habari za jumamosi wapendwa wasomaji wa blog hii na leo kitaa kimetembelea kikundi cha KANDANDA ndani ya facebook na kukutana na mjadala unaozungumzia waandishi wa habari za mchezo mjadala uliofunguliwa na MKUBWA KAMBI.

Twende kitaani:

MKUBWA KAMBI:
Ndugu zangu wana kandanda, humu ndani tumebahatika kuwa na waandishi wa habari, kwa muda mrefu sasa tumeshindwa kupata mahali pa kukutana nao, na kuwapa yale ambayo tunadhani ni mapungufu yanayoweza kuonekana kwa jicho la kawaida. Nina imani wengi wetu humu si wanasiasa, na huwa tunapenda kusoma habari za michezo, Mathalan leo nimenunua gazeti la Dimba kwenye ukurasa wa tatu kuna kichwa cha habari "Ngao ya Hisani pia bao", hiyo habari inazungumzia mchuano wa ngao ya hisani kana kwamba inachezwa wiki ijayo.
Hivi ngazi ya mhariri huwa ni nini?


FRANK ROBERT RWEYEMAMU:
Dah! Kaka Mkubwa Kambi, nasikitika kusema kuwa nimeacha kununua haya magazeti muda mrefu kidogo, nadhani uwepo wa KANDANDA group with active members in sports kumechangia sana mimi kuyatosa haya magazeti, lakini pia ukosefu wa umakini kwa hawa waandishi ndo sababu kubwa.


MOHAMED MKANGARA:
usahihi kidogo bwana Kambi halikuwa Dimba bali Bingwa, kwa kweli nimesikitika sana nilipokutana na habari ya namna hiyo hasa kwa gazeti la michezo, kwa bahati nzuri nimeongea na mhariri wa gazeti hilo na kumfikishia kilio hicho maana mi mweny ewe ilinichefua sana hiyo habari ila alinipa utetezi kuwa wakati wa kutayarisha gazeti msanifu kurasa alipaste vibaya,ila hilo nalo ni tatizo pia yaani ukosefu wa umakini na husababisha jamii kupata upotoshaji.


KAKA OMMY:
tumekosa waandishi kwa kweli tuna mashabiki tu hivi sasa cjaion hiyo ila lalamiko la wengi ni tuhuma achan na hayo magazeti kaka ayapo fair


MKUBWA KAMBI:
Kaka mkangara, yaani kusinge kuwepo ninyi wachambuzi kwenye haya magati nina imani wangenunua wauza maandazi, kuna kipengele kinachoitwa aliyebobea utakuta mchezaji habari yake imeandikwa kitambo inarudiwa kila wakati, ndugu zanguni sisi tun ataka habari mpya, si zile zinazojirudia, shukurani kwenu nyoote mnaoandika makala za uchambuzi kenye magazeti haya, hapa nitawatajha kwa uchache, Aloyce Komba, Mkangara, Kumwembe, Momburi,Maestro na wengineo, kwa kutumia group hii watanyooka, nina imani ulevi ndio unaowakosesha muda wa kuandaa na kuhariri habari


MOHAMED MKANGARA:
Unachokisema ni sahihi,kuna tatizo kubwa sana kwa waandishi wa michezo hilo nalifahamu kwa kuwa nimeshawahi kukaa kwenye media kwa muda mrefu na hivi sasa ninadhamana ya kuwaongoza waandishi hao,hilo gazeti ndio lilikuwa gazeti langu la kwanza kuliandikia na nakumbuka mpaka naachia ngazi na kwenda kuongeza elimu zaidi lilikuwa ni moja ya magazeti bora kabisa ya michezo nchini, why?

kulikuwa na waandishi waliomakini si kama makosa hayakuwapo la hasha lakini tuliyafukia kwa kutoa makala na habari zenye mvuto.


JOSE LUCAS MATO:
Mi sijui watanzania nafuu yetu iko wapi. Hakuna sehem tunaweza japo kujivunia kidogo! Magazeti ya michezo yananisikitisha sana. Sasa imefikia hatua nakua napata wasiwasi na uwezo na uelewa wa kawaida kuhusu waandishi.

Inaskitisha kwamba ugo njwa huu umelikamata hadi gazeti ambalo nililiamini nakulitumia mara nyingi yaan Mwanaspoti. Kkuna mda wanaandika vitu tofauti kabisa na ukweli ulivo, tena Front page. Mfano hai zaidi ni mwanaspoti ya tar23-26 , uk wa 21 . Wameandika eti Arsenal inakutana kesho(J'5 tar 24) na Olimpique Lyon badala ya Udinese! Sasa msomaji unaanza kujifikiria...

Hivi mwandishi anakua amelewa au..? Hivi inakuaje kosa kama hili linafanywa na mwandishi wa habari husika, linapita kwa mhariri, linapita kwa bodi za uhakiki, nk na tena unakutana na kosa kama hilo kesho yake na kesho yake na keshooo...

Hivi kweli hapa utasema kuna chama makini cha waandishi wa habari? au ni kipi hasa kinachofanyiika? Hii nchi hata tukipimwa kwa ligi za kufukuza kuku, bado tutakua mikia. Hivi hii nchi ilikiepo kwenye plan za Mungu kweli!!!!? make inachosha et!


EMMANUEL MAKUNDI:
@mkubwa kambi, sio hayo magazeti tu, ila kuna jamaa mmoja nimemsikia 92.9 fm akifanya interview na Nyambua halafu anaanza kumkejeli Interviwer sasa sijui inakuwaje kitaaluma? nadhani kuna haja ya kuwa na waandishi waliosomea profession hii haswaaaa!!lasivyo tunakoelekea hata injia ataanza kuandika habari za michezo.


KISININI PHILEMON:
mi niloishaacha kabisa kununua hayo magazeti mana ni mizinguo tu unakuta wanapiga porojo zisizo na maana ilimradi wanajaza habari kwenye gazeti na kuliuza, wanajali pesa kuliko usahihi wa habari, kwakweli wasipojisahihisha tunakoelekea hatutafika



kandanda group on facebook

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.