TIMU ya netiboli ya JKT Mbweni ilikamilisha michuano ya netiboli hatua ya makundi jana kwa kuitoa Mafunzo ya Zanzibar kwa magoli 54-41 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kutokana na matokeo hayo, JKT imemaliza hatua hiyo kwa historia ya kipekee ya kutopoteza hata mchezo mmoja tangu michuano hiyo ianze mapema wiki hii.
Timu hiyo inatarajiwa kuchuana katika hatua ya nusu fainali dhidi ya Uganda Prisons katika mchezo utakaochezwa leo asubuhi kwenye uwanja huo wa Taifa.
Akizungumzia ushindi huo, Kocha Mkuu wa JKT Mbweni, Mary Frank alisema mashindano yalikuwa ni mazuri kwa vile timu yake imecheza kama ambavyo alielekeza.
Alisema ana imani inaweza kuchukua ubingwa kama itaendelea na moto iliyoanza nao. Naye Kocha wa Mafunzo, Hidaya Abdulrahim alilalamikia marefa kutochezesha mchezo huo kwa haki, akidai kuwa hawakuwa makini.
Timu nyingine ambazo zitacheza hatua ya nusu fainali ni Polisi Uganda ambao walimaliza mchezo wa jana kwa kuwatoa wenzao wa nchi hiyo, KCC kwa mabao 41-33.
Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Prisons ya Kenya dhidi ya Kampala University wakati MOICT ya Kenya itacheza dhidi ya NIC Uganda
CHANZO: HABARI LEO

0 comments:
Post a Comment