Simba, Yanga kucheza na SOFAPAKA mwisho wa juma
Vigogo wa Soka Tanzania, Klabu za Yanga na Simba, wikiendi hii zitapata nafasi ya kucheza na Timu ngumu kutoka Kenya, Sofapaka, kwa mechi za kirafiki zitakazochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Akithibitisha habari hizi, Muandaaji wa ziara ya Sofapaka, Salum Mkemi, amesema Sofapaka itawasili Dar es Salaam Siku ya Alhamisi na Jumamosi watacheza na Yanga na Jumapili kuivaa Simba.
Mkemi pia alithibitisha kuwa tayari wamesharuhusiwa na Serikali kuutumia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hizo ambazo zitawasaidia Yanga na Simba kujipima na kujiandaa kwa michuano yao ya Barani Afrika ya CAF na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara unaoanza Januari 21.
Klabu ya Yanga tayari imethibitisha kucheza na Sofapaka kwa mujibu wa Afisa Habari wao Luis Sendeu.
Mkemi pia ametangaza Viingilio vya mechi hizo ambavyo ni Shilingi 2,000 kwa Majukwaa ya Kibuluu na Kijani, 3,000/= kwa Jukwaa la Machungwa, 8,000/= kwa VIP B na C na 10,000/= kwa VIP A.
Soka in bongo
0 comments:
Post a Comment