Mashabiki wa Simba wameshindwa kuujaza Uwanja wa Azam maarufu kama Ukumbi wa Harusi hapo jana na umeingiza mil 16 katika mchezo wa Kwanza wa Simba ndani ya uwanja huo.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura, Mechi hiyo ya ligi kuu ya Vodacom kati ya Simba na Polisi Dodoma imeingiza sh.16,839,000.
Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 2,257 ambapo kiingilio kilikuwa sh, 7,000 kwa mzunguko na sh. 20,000 kwa VIP. Waliokata tiketi za sh.20,000 walikuwa 80.
Baada ya kuondoa gharama za mchezo na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 2,568,661.02 kila timu ilipata sh.3,546,671.90. Mgawo mwingine ulikwenda kwa uwanja (sh. 1,162,893.90), TFF (sh. 1,162,893.90), Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF (sh. 581,446.95), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam- DRFA (sh. 465,157.56) na Baraza la Michezo la Taifa- BMT (sh.116,289.39).

0 comments:
Post a Comment