Wakati timu ya Taifa, Taifa stars ikiendelea kupoteza mvuto machoni mwa mashabiki wengi huku ikiwa inamvuto kwa baadhi ya wachambulizi wa soka la bongo, chini ya kocha Jan Poulsen. Tanzania imezidi kuporomoka katika viwango vya soka vinavyo tolewa na FIFA.
Tanzania ambayo ilikuwa inashika nafasi ya 125 na sasa inashika nafasi ya 126 kwa mujibu wa viwango vilivyotolewa jana na FIFA.
Mashabiki na wachambuzi walipishana katika kutoa maoni juu ya mchezo uliochezwa Taifa kati ya Taifa Stars na Algeria na mchezo kumalizika kwa sare ya goli moja kwa moja.
Wachambuzi wengi walionekana kuridhika kwa kiwango kilicho onyeshwa na Taifa Stars wakati mashabiki wakiponda.
Toka kuja kwa Kocha Jan Poulsen na kufanikiwa kutwa kombe la Challenge hapo mwishoni mwa mwaka jana, Tanzania imekuwa ikiporomoka katika viwango vinavyo tolewa na FIFA.
0 comments:
Post a Comment