vilabu

Mwalala akabidhiwa Coastal union


CALVIN KIWIA

MKENYA Ben Mwalala amekenua meno yote baada ya kurithishwa mikoba ya Jamhuri Kihwelo 'Julio' kukinoa kikosi cha Coastal Union ya Tanga.

Mshambuliaji huyo aliyewahi kukipiga na Yanga alisema jana Jumatatu kuwa ni takribani wiki mbili sasa amekuwa akiongoza mazoezi ya timu hiyo inayojiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

"Nimevutiwa zaidi na jinsi wenzangu walivyo makini na programu ya mazoezi, mwanzo nilifikiri wangeleta masihara, changamoto zipo isipokuwa sina jinsi ya kuzikabili kwa nguvu zote mara moja," alisema Mwalala.

"Mambo yataenda yakinyooka moja baada ya jingine na naamini tutakuwa na ushiriki mzuri zaidi," aliongeza.

Alisema amekuwa akiwasiliana na Julio kwa njia ya simu kila wakati kwa ajili ya kupata maelekezo zaidi.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Edo Kumwembe, alisema sababu za kumpa majukumu hayo Mwalala nikutokana na kocha Julio kuwa safarini nchi za Falme za Kiarabu huku msaidizi wake Juma Mgunda akikabiliwa na matatizo ya kifamilia.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.