KITAA:NANI MWENYEJI KATI YA RUVU SHOOTING NA MTIBWA SUGAR HAPO KESHO

Kikosi Cha Ruvu Shooting msimu uliopita

Ruvu Shooting yenye maskani yake mkoani Pwani hutumia uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi na uwanja wa Taifa kama uwanja wake wanyumbani wakati Mtibwa Sugar hutumia uwanja wa Manungu na Jamuhuri yote ya Morogoro na timu hizo zinataraji kukutana kesho katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi.

Mchezo huo wa Ligi kuu ya Vodacom inayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini unatarajiwa kurushwa moja kwa moja kupitia kituo cha Super sport 9, lakini swali linakuja ni nani mwenyeji wa pambano hilo?

Katika ratiba ya Ligi kuu ya Vodacom ina onyesha mwenyeji atakuwa Ruvu shooting wakati Ruvu shooting wakiwa wanatumia uwanja wa Mabatini na wa Taifa.

Nimekuwa nikijiuliza kitu gani kilichopelekea mchezo huo kutarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Azam badala wa ule wa Mabatini.

Tukirejea msimu uliopita katika mzunguko wa Kwanza Simba SC waliweka pingamizi ya kucheza na Azam FC katika uwanja wa Mkwakwani wakati uwanja wa Taifa ulikuwa umefungwa kwa madai sheria ya ligi hairuhusu timu kuwa na viwanja viwili vya nyumbani katika mikoa miwili tofauti, ambapo Azam FC walichagua kutumia uwanja wa Mkwakwani wa Tanga na Azam Complex uliopo jijini Dar es salaam.

Pingamizi la Simba SC lilipelekea kutangazwa kutumika kwa uwanja wa Azam katika pambano hilo, lakini kabla ya siku ya mpambano huo Serikali waliruhusu kutumika kwa uwanja wa Taifa.

Nilipo ukumbuka mkasa huo nikajenga hoja nyingine iweje Ruvu Shooting watumie uwanja wa Taifa wa jijini Dar es salaam na ule wa Mabatini uliopo Pwani kama viwanja vyake vya nyumbani katika ligi ambayo Simba waliiwekea pingamizi Azam kutumia Mkwakwani na Uwanja wa Azam.

Turudi katika mjadala wa kwanini mchezo wa Ruvu shooting na Mtibwa Sugar uchezwe katika uwanja wa Azam, uwanja ambao autumiwi na timu yoyote ile kama uwanja wake wanyumbani.

Sababu ambayo inayoweza kutolewa ni kwa sababu unarushwa moja kwa moja na Super sport. Pamoja na hivyo hakukua na haja ya kuutoa Mchezo Mabatini na jua hao Super sport kama walivutiwa kuonyesha mchezo huo wangeufuata.

Kwa mantiki ya kwamba tukifanikiwa kuingia nao mkataba si kila mchezo utakao rushwa na Super sport ufanyike Dar.

Ni wakati wa TFF na kamati zake kuheshimu taratibu na kanuni wanazo jenga la sivyo kamwe hatutoweza kufanikiwa katika soka letu

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.