Uhakika wa kuwepo burudani hiyo kamili toka kwa mapacha hao watatu katika soka inakuja baada ya yanga kukubali kumuachia kiungo Franky Dumayo ambaye akikutana na Salum Aboubakary (Sure boy) wa azam na Mwinyi Kazimoto wa simba huunda mapacha wa tatu wapinzani.
Dumayo anayesifika katika kutuliza kasi ya mashambulizi ya timu pinzani huku Sure boy akisifika katika kuichezesha timu na Kazimoto katika upigaji wa pasi za mwisho kwa pamoja hupelekea mashabiki kuridhika kwa kiingilio walicho tozwa baada ya kushuhudia wachezaji hao watatu wanao kutana kwenye thmu ya taifa pekee..
Nnje ya Dumayo Yanga wamemruhusu pia Kelvin Yondani wanaotarajiwa kuungana na wenzao kabla ya mchezo huo.
Kikosi cha stars kitakacho ondoka kesho kinaundwa na:
JUMA KASEJA, SALUM AISHI, AGGREY MORIRE, ERASTO NYONI, SHOMARI KAPOMBE, AMIR MAFATAH, KELVIN YONDAN, ISSA RASHIDI.
SALUM ABUBAKARY, MCHA KHAMISI, FRANKY DOMAYO, SHABAN NDITI, MWINYI KAZIMOTO, AMIR KIEMBA
MRISHO NGASSA, MBWANA SAMATA, THOMAS ULIMWENGU
0 comments:
Post a Comment