wachezaji

KASEJA HAIKIELEWWEKI LUPOPO

Na Clezencia Tryphone

HESABU za kipa Juma Kaseja kujiunga na FC Lupopo ya DR Congo, zimeanza kutibuka kutokana na mawasiliano duni baina yake na viongozi wa klabu hiyo kwa sasa, hivyo nyota huyo kutojua hatima yake katika msimu huu.

Kaseja alisema jana hadi sasa hajui kinachoendelea kutokana na wakala wake kutoka Lupopo, Ismael Bandua, kuwahi kushikiliwa nchini kwa kosa la kuwepo bila kibali na tangu kwisha kwa suala hilo, hajawa na mawasiliano naye.

Kaseja alisema baada ya kutakiwa kubadilishwa mkataba wake ambao alikuwa bado hajamwaga wino kutoka lugha ya Kifaransa na kuwa Kingereza, ndipo wakala wake Bandua alipokamatwa, hivyo suala lake kukwama na hajui itakuweje.

“Mimi mpaka sasa sijui kinachoendelea, kwani sina mawasiliano nao, tangu alipokamatwa wakala kwa kukosa kibali ndipo nilipoanza kukosa mawasiliano,” alisema Kaseja.

Alipouliza juu ya hatma yake baada ya kujitokeza hali hiyo, bado Kaseja akasema hayuko tayari kuzungumza lolote:

“Unauliza kwa kunitega, tukomee katika suala hili la mkataba, mengine we yaache tu, siwezi kusema lolote kwa sasa,” alisema Kaseja.

Baada ya wakala huyo kushikiliwa na Uhamiaji, alitakiwa kutumikia kifungo cha miezi mitatu jela au kulipa faini ya shilingi 150,000, sharti ambalo alilitimiza na kuachiwa, lakini kukiwa na ukimya wa kile kinachoendelea juu ya mpango huo.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.