Na Ezekiel Kamwaga, Simba SC
KLABU
ya soka ya Simba SC ya Dar es Salaam imefanikiwa kumuunganisha mchezaji
wake, Shomary Salum Kapombe, na klabu ya soka ya AS Cannes ya Daraja la
Nne nchini Ufaransa.
Mwenyekiti
wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage, amesema kwamba katika mkataba huo
mpya na wa aina yake kuwahi kufanywa na klabu yoyote ya Tanzania, Simba
imekubali mchezaji huyo achezee timu hiyo iliyo katika ligi daraja la
nne la Ufaransa kwa makubaliano ya kumtafutia timu ya kucheza ndani ya
miaka miwili kutoka sasa.
Rage ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), amesema timu hiyo itamgharimia Kapombe kwa kila kitu wakati atakapokuwa nchini Ufaransa na endapo atauzwa kwenda katika timu nyingine yoyote, Simba itapata gawio lake kupitia mauzo hayo na lengo la mchezaji huyo kubaki Ufaransa ni pia kumtengeneza awe bora zaidi kuliko alivyo sasa.
Rage ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), amesema timu hiyo itamgharimia Kapombe kwa kila kitu wakati atakapokuwa nchini Ufaransa na endapo atauzwa kwenda katika timu nyingine yoyote, Simba itapata gawio lake kupitia mauzo hayo na lengo la mchezaji huyo kubaki Ufaransa ni pia kumtengeneza awe bora zaidi kuliko alivyo sasa.
“Kwenye
makubaliano hayo, Simba haitapata chochote kwa sasa. Isipokuwa endapo
Kapombe atapata timu, Simba itapata mgawo wake kutoka katika mauzo hayo.
Makocha wa Ulaya wamebaini kwamba Shomari ni mchezaji mzuri sana lakini
anahitaji kuboreshewa vitu vichache kabla hajawa mchezaji mkubwa wa
kutumainiwa na vilabu vikubwa,” alisema Rage.
Rage
alisema katika mkataba huo mpya wa Kapombe, Simba imeangalia zaidi
maslahi ya taifa na ya mchezaji kuliko ya klabu kwa vile kama mchezaji
huyo atapata nafasi Ulaya, hilo litafungua milango kwa wachezaji wengi
wa Kitanzania ambao kwa sasa hawapati fursa Ulaya.
Wakala
wa Kapombe, Denis Kadito, alisema ingawa Kapombe ameonekana kuwa
mchezaji mzuri, kutofahamika kwa jina la Tanzania kumekuwa kikwazo
kikubwa kwa kupata kwake nafasi ya moja kwa moja na ndiyo maana imebidi
aanzie kwenye hatua ya chini.
“Ofa
hii ya Cannes ni nzuri kwa sababu timu hiyo huwa inacheza na timu za
akiba za vilabu vyote vinavyoshiriki katika Ligi Kuu ya Ufaransa na
hivyo atakuwa anaonwa na mawakala wa timu kubwa kila wiki. Hii
itamsaidia kupata timu kubwa mapema ndani ya msimu mmoja kutoka sasa,”
alisema Kadito.
AS
Cannes ni mojawapo ya vilabu vikubwa nchini Ufaransa na ni maarufu kwa
kuibua vipaji vikubwa. Miongoni mwa nyota maarufu wa Ufaransa waliowahi
kupita katika klabu hiyo ni Patrick Vieira, Zinedine Zidane na Luis
Hernandez.
Klabu
hiyo inafahamika kwa kuwa na miundombinu imara ya kumwezesha mwanasoka
kijana kukuza uwezo wake na ni matarajio ya Simba Sports Club, Kadito,
Cannes na Kapombe mwenyewe kwamba atakuwa mchezaji bora zaidi kuliko
sasa katika kipindi cha mwaka mmoja kutoka sasa.
Kutokana
na mkataba huo wa Kapombe na Cannes, Simba sasa imeongeza mkataba wake
na mchezaji huyo kwa muda wa miaka mitatu zaidi, kwa vile mkataba wake
wa sasa unamalizika Aprili mwakani. Kama Kapombe hatafanikiwa kupata
timu katika kipindi cha miaka miwili kutoka sasa, atarejea katika klabu
ya Simba kuendelea na majukumu yake.
0 comments:
Post a Comment