Na Boniface Wambura, TFF
WAGOMBEA wawili walioomba kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu wamewekewa pingamizi.
Waliopingwa ni Wallace John Karia anayeomba kupitishwa kuwania urais na Vedastus Kalwizira Lufano anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda Namba Mbili ambayo ni mikoa ya Mara na Mwanza. Anyempinga Karia ni Shamsi Rashid Kazumari wa Dar es Salaam wakati Lufano anapingwa wa Samwel Nyalla wa Mwanza.
Pamoja na mambo mengine, Kazumari anampinga Karia kwa madai kuwa akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, aliwashawishi wajumbe wenzake kuingia mkataba na Azam Tv wakati akijua kamati hiyo ni ya muda, hivyo haina nguvu za kisheria kusaini mkataba huo.
Naye
Nyalla ambaye pia ni mmoja wa wanamichezo waliojitokeza kuwania ujumbe
kupitia Kanda hiyo anampinga Lufano kwa madai hana uzoefu wa miaka
mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbezeleni itakutana
kesho (Agosti 28 mwaka huu) saa 4 kamili asubuhi kusikiliza pingamizi
hizo ambapo wawekaji pingamizi na waliopingwa wanatakiwa kufika wenyewe
ndani ya muda kwa vile uwakilishi hautakiwi.
Katika
hatua nyingine, Sekretarieti ya TFF inaendelea na maandalizi ya Mkutano
Mkuu wa Uchaguzi utakaofanyika Oktoba 26 na 27 mwaka huu jijini Dar es
Salaam.
Awali
mkutano wa uchaguzi ulikuwa ufanyike Februari 23 na 24 mwaka huu lakini
tukauahirisha kusubiri maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA), hivyo tayari wajumbe wana taarifa rasmi kuhusu mkutano
huo.
Orodha
ya wajumbe iliyotumwa awali kwa ajili ya Mkutano tunayo, isipokuwa kama
kuna wanachama wetu wana mabadiliko ya majina ya wajumbe
watakaohudhuria wanatakiwa kutuma majina hayo kabla ya Septemba 30 mwaka
huu.
Wanachama wa TFF ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu 14 za Ligi Kuu ya Vodacom.
0 comments:
Post a Comment