CAF

YALE YALE STARS WACHAPWA VIWILI

Lile gundu la Jan Poulsein limeendelea kumkumba Kim Poulsein baada ya leo Taifa stars kuendelea kupoteza michezo ya ugenini ya kusaka tiketi mbalimbali za michuano ya CAF na ya FIFA.

Taifa Stars ikicheza bla ya nyota wake Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanao itumikia timu ya TP Mazembe ya DR Congo wamekubali kichapo cha goli 2-0 toka kwa Gambia.

Katika mchezo huo uliochezwa nchini Gambia, wenyeji waliandika goli lake la kwanza katika dakika ya 44 kupitia kwa Mustapha Jarjue, goli lililo wapeleka wenyeji hao mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.

 Taifa stars ambayo leo pia walimkosa kiungo wake SalumAbubakary pamoja na mabeki Aggrey Morice, Shomar Kapombe, Kelvin Yondani kitendo kilichopelekea kiungo Henry Joseph kucheza nafasi ya beki.

Alikuwa yuleyule Mustapha Jarjue aliyeiandikia goli la pili Gambia katika dakika ya 51, na kupelekea mchezo kumalizika kwa Gambia goli 2-0.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Stars kumaliza wakiwa wa tatu wakijikusanyia point 6 huku Gambia wakiwa wa mwsho katika kundi hilo la C kwa kujikusanyia point 4.

Katika kundi C Ivorycoast ndio timu iliyofanikiwa kufuka hatua ya makundi na kuingia katika hatua ya mwisho wa kusaka timu 5 zitakazo wakilisha bara la Africa katika michuano ya kom,be la Dunia.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.