riadha

40 KWENDA NNJE KUJIANDAA NA MADOLA

RIADHA Tanzania (RT) wametangaza majina 40 ya awali kwa ajili ya kambi za mazoezi nje ya nchi kushiriki Michezo ya 20 ya Jumuiya ya Madola mwaka huu na ile ya Olimpiki 2016.

Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui alisema Dar es Salaam jana kuwa wanariadha hao wamegawanywa katika makundi matatu, na watapiga kambi katika nchi za Uturuki, China na Ethiopia.

Ofa hiyo ya kupiga kambi nje ya nchi imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ili kuiwezesha Tanzania kurejea na medali kutoka katika michezo hiyo.

Kwa mujibu wa Nyambui, wanariadha watakaopiga kambi Uturuki ni Michael Nkungu, Nelson Mbuya, Selina Amos, Jenipher Mollel na Mariam Salum.

Wengine watakaokwenda Uturuki kwa kambi ya mbio fupi na zile za kati ni Damian Chopa, Sebastian Mohere, Michaekl Zacharia, Michael Mang’unyila wakati makocha ni Samuel Tupa na Yussuf Nassoro.

Wanariadha watakaokwenda kwa ajili ya kambi ya mbio za kati na mitupo nchini China ni Taratibi Hozza, Hassan Khamis Ali, Adnan Chongoe, Keneth Maluba, Ali Khamis Ghulam, Imani Rusanganya, Silvestre Naali, Atson Kwilomba, Said Makula, Msiwa Lamech, Jeremia Chacha, Peter Nyamngono na Benjamin Kulwa.

Wengine ni Yakobo Sirima, Hafidh Hafidh, Gideon Msoni, Dotto Ikangaa na Ally Seif Juma wakati makocha wao ni Boniface Ngukulu, Oswald Kahuruzi, Dickson Marwa na Hamisi Mohamed Ally.

Wanariadha watakaokwenda Ethiopia kujiandaa kwa mbio ndefu ni Alfonce Felix, Ezekiel Jaffer, Ismail Juma, Catheline Lange, Jacquline Sekilu, Sarah Ramadhani, Samson Ramadhan, Faustine Mussa, Daud Lwambe, Paschal sarwat.

Makocha wa timu hiyo yenye nyota kibao wa riadha ni Michael Washa na Shabani Hiki. Kwa mujibu wa Nyambui, kambi hizo zitaanza baadaye mwezi huu.


chanzo: habari leo

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.