simba

KIBADENI AREJEA SIMBA KAMA MAKAMU

Raisi wa Simba SC, Evans Aveva  amemrejesha  klabuni Abdallah Kibaden Mputa kama makamu mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya Simba SC, baada ya kuitumikia Simba SC kipindi cha nyuma kama mchezaji na kocha.

Kibaden mara ya mwisho kuwa Simba SC ni mwaka jana desembr ambapo aliiongoza Simba SC katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya vodacom msimu wa 2013/14 kama kocha mkuu wa timu hiyo.

Aveva leo ametaja Kamati ndogo ndogo ndani ya Simba SC ambapo kamati ya ufundi itakuwa inaongozwa na Collin Frisch, makamu wake akiwa ni Kibaden. Wajumbe wa Kamati hiyo ni Mohamed Yakob, Patrick Rweyemamu, Othman Kazi, Geiorge Lucas na Duwa Said.

Wakati kamati ya usajili ikiendelea kuwa chini ya Zacharia Hans Poppe ataendelea kuongoza Kamati ya Usajili, Makamu wake akiwa ni Kassim Mohammed Dewji na Wajumbe Crescentius John Magori, Said Tulliy, Collin Frisch, Musleh Al-Rawahi na Rodney Chiduo.
 
Kamati ya Mashindano Mwenyekiti ni Mohamed Nassoro ‘Steven Seagal’, Makamu wake Idd Kajuna na Wajumbe Gerald Yambi, Hamphrey Mkumbo, Bituro Kazeri, Juma Ndambile, Hemed Milanzi na Abdul Salehe.

Kamati ya Soka la Vijana Mwenyekiti ni Said Tulliy, Makamu wake Juma Pinto Wajumbe na Wajumbe Amina Poyo, Mulamu Nghambi, Juma Ndambile, David Kivembele, Hemed Omary na Rehule Nyaulawa.

Kamati ya Fedha Mwenyekiti: Geofrey Nyange 'Kaburu', ambaye pia ni Makamu wa Rais wa klabu, Makamu Aziz Kefile na Wajumbe Jasmine Badouh, Muhada Engbert, Nicky Magarinzi, Mchalange France na Ally Suru.

Kamati ya Maadili Mwenyekiti ni Samson Mbamba, Makamu Hassan Tikka na Wajumbe Peter Muinzi, Gerlad Mongella na Hassan Mnyenye.

Kamati ya Nidhamu Mwenyekiti ni Michale Ngallo, Makamu Said Hemed El Maamry na Wajumbe Fotonatus John Mangwela. Ismail Mohamed na Ngasa Ganja.

Kamati ya Masoko Mwenyekiti ni Salim Abdallah ‘Try Again’, Makamu wake Crescentus Magori na Wajumbe Azim Dewji, Musleh Al Rawahi, Iman Kajula, Juma Pinto, Farough Baghoza na Ruge Mutahaba.

Kamati ya Wanachama na Matawi Mwenyekiti wake Kassim Dewji, Makamu Idd Kajuna na Wajumbe: Mulamu Ngh'ambi, Masoud Hassan, Abdul Mshangama, Omary Mkonje, Albino Lwila, Hassan Mkande, Hussein Simba, Yahaya Athuman, Hassan Kaniki, Bakary Ngurumo, Seydou Rubei, Manesh Rupareria, Omary Makamba, Omary Makoye, Said Kubenea, Shaaban Nyaa, Abdulkarim Juma, Msumari Mbwana, John Bondo na Bakary Mnyachi.

Aveva pia ametaja Kamati ya Muda ya Matamasha ya klabu chini ya Mwenyekiti Gerald Yambi, Makamu Mulamu Ngh'ambi na Wajumbe Dk Mohammed Wandi, Jasmine Badour, Said Nembo, Peter Richard na Ramadhan Hamisi.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.