mingine

MBIO ZA VEISAKHI KUTIKISA MOSHI

MJI wa Moshi mkoani Kilimanjaro utakuwa kwenye burudani ya mwaka ya mashindano ya magari yajulikanayo kama Vaisakhi Rally yatakayofanyika Jumapili wiki hii.

Msimamizi mkuu na mwandaaji wa mbio hizo za magari, Faheem Aloo akizungumza na vyombo vya habari jana hapa, alisema maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika na ukaguzi wa njia umekamilika, na zitaanzia na kuishia eneo la KIA Bomang’ombe wilayani Hai.

“Kila kitu kimekamilika na suala zima la njia ambazo magari hayo yatapita zimekaguliwa na zipo tayari na salama kwa madereva kuoneshana ujuzi siku hiyo ya Jumapili,” alisema Aloo.

Alisema mashindano hayo yatakuwa tofauti na yale yaliyozoeleka kwani yameongezwa vitu vingi ambavyo vitashindaniwa kama vile dereva atakayeweza kurusha gari juu vizuri, atakayezungusha gari kwa kasi vizuri, atakayepita kwenye maji kwa mbwembwe vizuri na gari itakayoonekana vizuri kwenye picha.

Aloo alisema madereva hao watapata zawadi maalumu kutoka kwa wadhamini ambao wamedhamini kila tukio kwenye mashindano hayo ya magari ambao ni Utrack Africa Ltd, Radio wave Communications Ltd, Maji Poa, Polaris, Kundan Enterprises, Sunvic, Soda King, SCCL, Simba Trucking, Security Group, Hari Sing and Sons.

Wengine ni 2M Media, Kalsi & Jutley Enterprises, Authentic Emergency Services, HAL, Tigo, Red Bull, AA Tanzania na Siera Zulu.

Aloo alisema katika mashindano hayo kila gari litakuwa likiangaliwa kwa mitambo maalumu ya kuangalia magari kwa mwenendo wake wote na kama litakuwa limepata shida yoyote porini na kupata msaada wa haraka kutoka kwa kitengo husika, kwa kuwezeshwa na Utrack Africa Ltd na hivyo kuyafanya mashindano hayo kuwa ya kisasa zaidi na salama.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.