
Shaffihdauda.com: Pole sana kwa mechi na hongera kwa ushindi
Awadh: Asante nashukuru
Swali: Unajisikiaje kufunga goli kwenyemechi siku ya Simba Day
Awadh: Nimefurahi sana kwasababu hii ndio mechi yetu ya mwanzo ambayo ndio siku yetu ya ufunguzi tumepata ushindi, perfomance na jinsi tulivyocheza, mwalimu wetu mpya kila mtu anajua tumefurahi kwa sasa, kwasababu bado tupo kwenye maandalizi naamini tutakuwa vizuri zaidi.
Swali: Unawazungumziaje waganda kwasababu wamecheza pungufu kwa muda mrefu lakini mmef anikiwa kupata ushindi dakika za mwisho?
Awadh: Kwakweli jamaa ni wazuri sana na sisi siku zote tunatafuta timu ambayo tunajua iko juu kwasababu mwalimu anajua nini anataka akaangalie hatutafuti timu ambayo tunajua iko chini yetu kwahiyo mwalimu ameona makosa yako wapi na mazuri yapi tumefanya lakini jamaa ni wazuri sana.
Swali: Unawaambia nini mashabiki wa Simba kuelekea michuano ya ligi kuu Tanzania bara?
Awadh: Tunamuomba Mungu kwanza atupe afya njema, kila mtu awe na afya njema mpaka ifike muda wa ligi kila mtu awe mzima kwasababu kila mtu anakiu ya kuwapa wana Simba kile wanachotaka kikubwa ni ushindi na mafanikio lakini wanasimba kwa muda mrefu wamekuwa wanasubiri kombe sio kitu kingine, sio nafasi ya pili ama yatatu na mwaka huu tunajipanga tuwape hiyo zawadi wanayoitaka kwa kuchukua ubingwa.
Shaffihdauda.com: Asante sana, hongera sana
Awadh: Asante, nashukuru pia.
Hapa nimekuwekea sauti ya Awadh, kuisikiliza bofya hapa chini upate stori nzima ilivyokuwa…
0 comments:
Post a Comment