Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars imekubali kufungwa goli 7-0 toka kwa Algeria katika mchezo wa marejeano uliochezwa nchini Algeria na kupelkea Stars kutolewa katika mbio za kusaka tiketi ya kushiriki kombe la dunia kwa jumla ya magoli 9-2.
Katika mchezo wa leo ambapo Al-geria walifunguka vilivyo na kuutawala mchezo watakavyo na kupelekea wahcezaji wa Stars kukosa utulivu.
Algeria waliandika goli la kwanza katika sekundi ya 36 kupitia kwa Yassin Ibrahim akimalizia pasi ya Selman Ismail.
Kuingia kwa goli hilo kulipoteza utulivu kwaTaifa Stars ambapo na kupelekewa kupewa kadi za njano wachezji wa nne ndani ya dakika 20 za mwanzo wa mchezo.
Katika dakika ya 23 Fauz aliiandikia Algeria goli la pili na katika dakika ya 36 Mudathir Yahya alizawadiwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
Katika daskika ya 43 Algeria waliandika goli la 3 kupitia kwa Riadh Mahrez na kuipeleka Algeria mapumziko wakiwa mbele kwa goli 3.
Katika kipindi cha kwanza Stars walifanikiwa kufika langoni mwa Algeria mara mbili ambapo moja walifanikiwa kutia mpira nyavuni lakini mwamuzi akalikataa hilo goli kwa madai Maguli alikuwa ameotea.
Mara ya pili Alikuwa Samatta ambapo shuti lake lilikuwa dhaifu na kupelekea kipa kudaka kirahisi, wakati Algeria wao walifanikwa kutengeneza nafasi y 4 katika kipindi cha kwanza na kutumia nafasi 3.
Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko kwa upande wa Taifa stars ambapo Mkwasa alimtoa Farid Mussa na nafasi yake kuchukuliwa na Salum Telela huku Aishi Manula akichukuwa nafasi ya Ally Mustafa Bathez.
Kalamu ya magoli ya ALgeria iliendelea katika dakika ya 48 kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Selman Islam kabla ya Fauz kufunga goli la 5 kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 68.
Katika dakika ya 70 Manula aliokoa michomo miwili mfululizo na kusababisha kona iliyozaaa goli 6 ambalo lilifungwa na Carl Merjan kbla ya Ghezal Rashid kuifungia Algeria katika dakika ya 74 goli la 7.
Katika kipindi cha pili Al-geria walitengeneza nafasi 8 na kuzitumia nafasi 4 huku Stars wakitengeneza nafasi mbili ambapo walishindwa kuzitumia na hivyo kupeleka mchezo kumalizika kwa Algeria kuibuka na ushindi wa goli 7-0.
Kwa matokeo hayo Taifa stars wameshindwa kutinga katika hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kushiriki kombe la dunia nchini Urusi..
0 comments:
Post a Comment