ASFC

MWADUI WAITNGA 16 BORA, MCHEZXO NUSURA UVUNJIKE, MASHABIKI WARUSHA MAWE


Mwadui FC wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya kombe la TFF linalo dhaminiwa na Azam Sports, baada ya kuwachapa Stand united goli 1-0, mchezo ambao amanusura ushindwa kumalizika baada ya mashabiki kuto ridhishwa na mwamuzi wa mchezo huo.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga,  ulishuhudia timu zikienda mapumziko wakiwa sare ya bila kufungana, huku kukitengenezwa nafasi chache za magoli katika kila upande.

Mwadui FC waliandika goli lao pekee katika dakika ya 71 kupitia kwa Jerry Teget kwa mkwaju wa penati uliotokana kusukumwa kwa Rashid Mandawa.

Katika dakika ya 88 mashabiki waliatahamaki baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya refa wa mchezo na kuanza kurusha mawe uwanjani kitendo kilichopelekea mchezo kusimama kwa mda. wa dakika 4 na baadae kuendelea na kumalizka kwa Mwadui FC kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Minogoni mwa maamuzi tata ya mwamuzi ni juu ya penati ya Mwadui na kukataliwa goli la Stand united katika dakika ya 86.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.