maproo

NGOMA AREJEA NA KUJIUNGA NA WENZAKE ZANZIBAR


Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Donald Ngoma amerejea nchini na tayari ameungana na kikosi cha timu hiyo kilichoko Pemba, Zanzibar kinachojiandaa na mechi yake ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya Azam FC itakayofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ngoma alikuwa kwao Zimbabwe kuhudhuria mazishi ya mdogo wake aliyefarika dunia kwa ajali ya kugongwa na gari mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kutokana na msiba huo, mshambuliaji huyo aliikosa mechi ya marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Cercle de Joachim kutoka Mauritius.

Akizungumza jana, Msemaji wa Yanga, Jerry Muro, alisema sasa kikosi chao kimekamilika na wanaamini wataendeleza kasi ya ushindi katika mechi zake zote zinazofuata.

Muro alisema Yanga imefurahishwa na tabia ya nidhamu iliyoonyeshwa na mchezaji huyo na anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa wachezaji wengine wa klabu hiyo.

"Ndiyo amerudi nchini leo na tayari ameshatua Pemba kuungana na wenzake," alisema kwa kifupi Muro.

Ngoma na Amissi Tambwe kutoka Burundi ndiyo wachezaji wanaoongoza safu ya mashambulizi ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Bara.

CHANZO: NIPASHE

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.