ASFC

AZAM WATINGA FAINALI KWA MIKWAJU YA PENATI


Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam FC wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya kombe la shirikisho la soka nchini TFF, linalodhaminiwa na dawati la michezo la Azam TV, (Azam Sports Federation Cup) baada ya kuiufnga MWadui kwa mikwaju ya penati 5-3.

Katika mchezo huo uliochezwa leo katika uwanja wa Mwadui mkoani Shinyanga ambapo mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika Azam FC walikuwa mbele kwa goli 1-0.

Katika kipindi hicho cha kwanza Mwadui FCwalipoteza nafasi tano za wazi walizotengeneza wakati Azam FC wakitumia nafasi moja kati ya tatu walizotengneza.

Katika dakika ya 4 Khamisi Mcha viali aliiandikia Azam FC goli la kwanza baada ya kumalizia mpira uliopozwa na Jean Baptisti Mugireneza kufuati krosi ya Erasto Nyoni.

Katika kipindi cha pili Mwadui FC walirekebisha makosa yao na kuitumia nafasi nafasi moja kati ya tatu walizo tengeneza na kupelekea dakika 90 zikimalizika kwa sare ya goli 1-1.

Goli la Mwadui FC lilifungwa katika dakika ya 82 kupitia kwa Hassana Salum Kabunda na kupelekea mchezo kwenda dakika 30 za nyonngeza.

Katika dakika ya 97 Khamisi Mcha akitumia uwezo wake binafsi aliiandikia Azam FC goli la pili kabla ya Mwadui FC kusawazisha kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 120 kupitia kwa Jabiri Azizi Stima.

Mchezo huo uliamuriwa kwa mikwaju ya penati na Azam FC wakipata penati zote tano, wakati mwadui wakipoteza penati moja na kupeleka mchezo kumalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 55-3.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.