KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania (Twiga stars) kinatarajiwa kuwekwa hadharani mwishoni mwa mwezi huu kwa ajili ya kuingia kambini siku 10 kabla ya mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya Taifa ya Rwanda huku wakipatiwa mwalimu maalumu kutoka nchini Rwanda kwa ajili ya maandalizi ya timu yake kuelekea katika mashindano ya fainali za mataifa ya Afrika kwa upande wa wanawake.
Rwanda ilituma mwaliko huo kutokana na kiwango kizuri walichokionesha Twiga katika michezo yake mbalimbali ya kimataifa waliyoicheza.
Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Alfredy Lucas amesema mchezo huo ni mwaliko maalumu kutoka kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa ajili ya kuwapa burudani viongozi watakaohudhuria mkutano mkuu wa nchi za Afrika AU.Mkutano huo unatarajiwa kuanzia Julai 14 mpaka 16 mwaka huu hivyo anataka kuonesha viongozi hao kuwa hata wanawake wanaweza.
Amesema, kwa kipindi kirefu wanawake wamechukuliwa kama viumbe dhaifu hivyo mchezo huo utasaidia kuondoa fikrea hizo.
"Tunatumai kuwa Twiga wataonesha kiwango kizuri katika mchezo huo na kuleta ushindani mkubwa ili kudhihirisha kuwa si wanaume tu ndio wanaoweza kusakata kabumbu bali hata wanawake wanauwezo mkubwa katika mchezo huo", amesema Alfred.
0 comments:
Post a Comment