TFF

23 WAITWA KUWAVAA ALGERIA

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars Salum Mayanga hii leo ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kitakocho cheza michezo miwili ya kirafiki mwishoni mwa mwezi huu.

Taifa stars wanataraji kucheza na Algeria machi 22, mchezo utakao chezwa nchini Algeriia, kisha kuja nchini kucheza na DR Congo machi 27.

Mechi zote hizo mbili zipo katika kalendaya shirikisho la soka duniani FIFA, na hiyo ndio inakuwa michezo ya kwanza kwa Taifa stars kucheza tangu mwaka huu uanze.

Wachezaji walio itwa ni Makipa Aisha Aishi manula,Abulrahman Mohammed,Ramadhani Kabwili, mabeki ni Shomari Kapombe,Hassan Kessy,Gadiel Michael,Kelvin Yondani,Abdi banda na Erasto Nyoni.

Viungo ni Hamis Abdallah, Mudathir Yahya, Said Ndemla,Faisal Salum, Abdulazizi Makame, Farid Mussa, Thomas Ulimwengu, Ibrahim Ajibu, Shiza Kichuya na Mohammed Issa na washambuliaji ni Mbwana Samata, Saimon Msuva, John Bocco na Yahya Zayd.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.