VPL

AZAM FC WAICHAPA SINGIDA UNITED, MWADINI AKIZIBA PENGO

Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam FC leo wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhibi ya Singida United katika muendelezo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Katika mchezo huo ulifanyika saa moja usiku katika uwanja wa Azam complex ulishuhudia Azam FC wakianza mchezo kwa kasi na mnamo dakika ya 7 amanusura wapate bao la kuongoza kupitia kwa Mbaraka Yusuph ambaye shuti lake ligonga mwamba.

Katikadakika ya 16 ya mchezo Joseph Mahundi aliiandikia Azam FC goli la kwanza akiunga pasi ya Mbaraka Yusuph goli lilodumu dakika zote 90 za mchezo.

Leo Azam FC kwa mara ya kwanza katika msimu huu ndani ya michezo ya ligi kuu ilicheza bila ya kipa wake namba moja Razak Abalora aliyefungiwa na TFF kucheza michezo ya ligi kuu ya vodacom mpaka shauli lake litakapo sikilizwa na kamati ya nidhamu.

Kipa aliyechukuwa mikoba ya Abalora leo, Mwadin Ally alifanya kazi ya ziada mara kadha kuzuia nyavu zake zisiguswe na kupeleka Azam FC kuvuna pointi hizo tatu ambazo zinawafanya wafikishe pointi 38 wakiwa nyuma ya yanga wenye pointi 48 na Simba SC wenye pointi 46.

Azam FC : Mwadini Ali, David Mwantika, Bruce Kangwa, Abdallah Kheri, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mbaraka Yusuph/Shaaban Iddi dk66, Yahya Zayed/Salmin Hoza dk90 na Joseph Mahundi/Ennock Atta Agyei dk30.

Singida United; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shafiq Batambuze, Miraj Adam, Salim Kipaga/Malik Antiri dk70, Kennedy Wilson, Kenny Ally, Deus Kaseke/Asad Juma dk66, Tafadzwa Kutinyu, Danny Usengimana, Kambale Salita na Kiggi Makassyas

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.