VPL

AZAM WAISHUHSA YANGA, MAJIMAJI HALI MBAYA

Mabingwa wa kombe la mapinduzi Azam FC hii leo wamefanikiwa kuwashusha yanga sc katika msimamo wa ligi kuu ya vodacom kutoka katika nafasi ya pili mpaka ya tatu baada ya kuifunga Mwadui FC goli 1-0 katika mchezo uliochezwa leo usiku katika uwanja wa Azam Complex.

Katika mchezo huo wa leo kama safu ya ushambuliaji ya Azam Fc ingekuwa makini ingetoka na magoli yasiyopunguwa matatu, ambapo walipoteza nafasi hizo kupitia kwa washambuliaji Benard Arthur alieingia kipindi cha pili na Yahya Zaydi.

Katika mchezo huo ulioshuhudia Mbaraka Yusuph akitolewa katika dakika ya 24 baada ya kuumia na nafasi yake ikachukuliwa na Shaban Iddi, Azam FC waliuwanza mchezo kwa kasi na kama Yahya Zayd angekuwa makini angeiandikia Azam Fc goli katika dakika ya 3 ya mchezo baada ya kupoteza nafasi ya wazi.

Yahya Zaydi mchezaji pekee toka Azam FC aliyejumuishwa katika kikosi cha Taifa stars kitakacho cheza na Algeria, aliandika Azam FC goli la kwanza katika dakika ya 5 ya mchezo akitumia vyema makosa ya safu ya ulinzi ya Mwadui FC goli liliodumu dakika zote za mchezo na kuwafanya Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Katika mchezo mwingine wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja Majimaji mkoani Ruvuma umeshuhuda Majimaji wakiendelea kuwa katika hali mbaya baada ya kupoteza kwa kufungwa goli 1-0 na Ndanda FC.

Goli hilo la Ndanda FC lilifungwa na John George na kuwafanya Ndanda FC kufikisha pointi 21 na kuwaacha Majimaji wakiendelea kubuluza mkia.

Na katika uwanja wa Samora mkoani Iringa Lipuli FC imeendelea kukimbia hatari ya kushuka daraja baada ya kuichapa Njombe Mji goli 2-1. Goli za Lipuli zikifungwa na Jerome Lambele na Adam Salamba huku goli la Njombe Mji likifungwa na David Obash.

MATOKEO YA MICHEZO YA LEO VPL

Stand United 0-0 Tanzania Prisons
Lipuli 2-1 Njombe Mji
Majimaji 0-1 Ndanda SC
Azam FC 1-0 Mwadui FC

MCHEZO WA KESHO VPL

Yanga SC Vs Kagera Sugar

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.