VPL

STAND WAITULIZA SIMBA TAIFA

Wachezaji wa Stand United na benchi la Ufundi
Stand United ya mkoani Shinyanga hii leo wameisimamisha Simba SC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam baada ya mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa leo kumalizika kwa sare ya goli 3-3 na kufanya Simba SC wanao ongoza ligi kuendelea kuongoza wakiwa na pointi 46 baada ya kucheza michezo 20 wakiwa wamewazidi wapinzani wao Yanga pointi 6 ambao wamecheza michezo 19 mpaka sasa.

Katika mchezo wa leo  uliochezeshwa na mwamuzi Florentina Zabron kutoka Dodoma akisaidiwa na Ferdinand Chacha na Mashaka Mandemwa wote wakitokea Mwanza, ulishuhudia dakika 45 za mwanzo zikimalizika kwa sare ya goli 2-2 ambapo Stand United walitoka nyuma na kusawazisha magoli yote mawili.

Simba SC walianza kusheherekea goli lao la kwanza katika dakika ya 6 kupitia kwa Asante Kwasi akimalizia mpira uliotemwa na kipa Mohammed Makaka kufuatia shuti la Laudit Mavugo.

Katika dakika ya 23 Simba SC walifanikiwa kuandika goli la pili kupitia kwa Mavugo akimalizia krosi ya beki wa kulia, Shomary Kapombe na kuipa ungozi Simba Sc wa goli 2-0.

Wakati Simba SC wakiamini kuwa yale yaliyo wakuta Mbao FC na Stand united itawakuta, walijikuta wakiruhusu magoli mawili ndani ya dakika 4, kupitia kwa Tariq Seif aliyeifungia Stand united goli la kwanza katika dakika ya 36 na dakika ya 40 Aron Lulambo aliisawazishia Stand united  na kupeleka mchezo kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 2-2.

Simba walianza kipindi cha pili kwa mabadiliko ambapo Mavugo alimpisha Juma Luizio, mabadiliko ambayo yalipeleka Simba Sc kuandika goli la tatu katika dakika ya 61 kupitia kwa Nicholaus Gyan.

Iliwachukuwa dakika 6 Stand kulipa kisasi cha kufunga goli la tatu katika mchezo huo kupitia kwa Mrundi Bigirimana Blaise kwa shuti kali kufuatia mpira wa kurushwa na beki wa kushoto, Miraj Maka na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 3-3.

Simba SC leo; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Asante Kwasi, Yussuf Mlipili, James Kotei, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Muzamil Yassin/Mwinyi Kazimoto dk74, Laudit Mavugo/Juma Luizio dk46, Shiza Kichuya na Nicholas Gyan/Moses Kitandu dk90+2.

Stand United leo; Mohamed Makaka, Aaron Lulambo, Miraj Maka, Erick Mulilo, Ally Ally/Abdallah Juma dk90, Abel Kassim/Ismail Gambo dk81, Bigirimana Blaise/Sixtus Sabilo dk70, Jisendi Mathias, Tariq Seif, Suleiman Ndikumana na Vitalis Mayanga.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.