aamsuni:
Mshambuliaji aliesajiliwa na yanga msimu uliopita na kushindwa kuitumikia klabu hiyo katika ligi kuu, Kenneth Asamoah anaweza kujiunga na simba endapo klabu ya Asante Kotoko ya Ghana na Simba wakiafikiana.
Akizungumza mjini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Rage alisema taratibu za Shirikisho la Soka la Kimataifa ( Fifa) zinazuia klabu kujadiliana na mchezaji moja kwa moja bila kuhusiana na usajili bila kupitia uongozi wa klabu anayoichezea. Kutokana na hali hiyo, Rage alisema si kweli kwamba Simba inafanya mazungumzo na mchezaji huyo, badala yake inachofanya sasa ni kuzungumza na klabu ya Asante Kotoko ambaye anachezea Asamoah.
Rage alisema wanatarajia kumtuma Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geodfrey Nyange ‘Kaburu’ kwenda Ghana kumalizia mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji huyo.

0 comments:
Post a Comment