Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa stars wamekubali kufungwa na South Africa 'Bafana bafana' goli moja bila katika mpambano wa kirafiki uliopigwa katika uwanja wa Taifa.
Katika mpambano huo wakujiweka sawa kabla ya mechi za kufuzu kwenda Gabon na Guine kushiriki michuano ya kombe la Africa, ziliwakosa nyota wake wanaokipiga nnje ya nchi.
Bafana bafana
walipata bao katika dakika ya 43 likitiwa nyavuni na Siyabonga Sangweni akiunganisha vyema mpira wakona ambao Juma Kaseja aliushinda kuzuiya.
Tanzania walishindwa kutengeneza nafasi za kutosha katika kipindi cha kwanza, na nafasi zilizojitokeza walijikuta wakizipoteza kupitia kwa John Boko, Julius Mrope na Mohamed Banka.
Kipindi cha pili Taifa stars walicheza kwa kuonana baada ya kuingia Mwinyi Kazimoto kuchukuwa nafasi ya Ramadhan Chombo, na kisha akamtoa Juma Kaseja na kuingia Shaban Dihile. Katika dakika ya 60 stars walikosa goli kupitia kwa John Bocco akishindwa kuunganisha krosi ya Shadrack Nsajigwa.
Taifa Stars walizidi kuwapoteza Bafana bafana katika dakika 15 za mwisho huku wakishindwa kutia mpira wavuni.
Stars huo ni mchezo wake wapili mfululizo kupoteza toka wamfunge Jamhuri ya Africa ya kati ambayo watakutana nayo hapo juni 4 katika harakati ya kusaka nafasi ya kushiriki kombe la mataifa Africa.
aamsuni

0 comments:
Post a Comment