TFF

TSA kuwekwa mezani

Kitua cha kulea wanakandanda, Tanzania Soccer Academy (TSA), kinasimamiwa na TFF pamoja na kampuni ya Kiliwood, kilisimamisha shughuli zake tangu mwaka jana. Na hivyo kupelekea Tff pamoja na kiliwood kupanga kukutana kukizungumzia.
Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura kwa waandishi wa habari inasema, kwa kuwa TSA iko chini ya TFF pamoja na Kiliwood inakuwa ngumu kwa TFF kulitolea maamuzi bila kuwashirikisha kiliwood na hivyo wako mbioni kukutana na kufikia muwafaka juu ya kituo hicho kilicho kuwa kinalea vijana kati ya miaka 17 na 20. “Kutokana na hali hiyo Sekretarieti kwa sasa inafanya mawasiliano na kampuni ya Kiliwood ili pande hizo mbili zikutane na kuelezana juu ya uamuzi wa Kamati ya Utendaji ya TFF juu ya mustakabali wa kituo hicho ambao kwa sasa hatuwezi kuuweka wazi mpaka pande hizo zitakapokutana,” ilieleza taarifa hiyo.
Katika taarifa hiyo iliendelea kwa kufafanua kuwa moja ya majukumu ya TFF katika mkataba kati yake na Kiliwood juu ya uendeshaji wa kituo hicho ilikuwa ni kutoa vitendea kazi (facilities) ambavyo ni hosteli na uwanja wa mazoezi.

Kituo hicho kimewatambulisha nyota mbali mbali akiwemo Thomas Ulimwengu aliyekwenda Harmburg nchini Ujerumani kwa ajili ya Majaribio pamoja na Omega Same anaekipiga Yanga.

Katika Taarifa hiyo pia ilieleza kuwa shirikisho hilo kupitia Kurugenzi ya Ufundi imeandaa kozi ya wakufunzi wa marefa wa mikoa itakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Juni 1 hadi 4 mwaka huu. Kozi hiyo ambayo mara ya mwisho ilifanyika hapa nchini mwaka 2008 inatarajia kushirikisha wakufunzi wa marefa zaidi ya 20 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.
Waendeshaji wa kozi hiyo watakuwa ni Stanley Lugenge ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya TFF, Leslie Liunda, Joseph Mapunda, Hafidh Ally na Juma Hamisi.


aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.