VPL

Mnyama kuwinda miwa ya Turiani

Ukiwa na Tsh 5000 inatosha katika kushuhudia mtanange wa ligi kuu ya vodacom katika uwanja wa Taifa kati ya Mnyama Simba na Wakata Miwa wa Turiani Mtibwa Sugar.

Patrick Mutesa Mafisango anatarajiwa kuendelea kuongoza kiungo cha Simba huku akisaidiwa na mkenya Jerry Santo mbele yao akicheza mtukutu toka Tanzania Haruna Moshi Boban.

Mafisango ndiye mchezaji wa simba aliyeshinda magoli mengi msimu huu akiwa na magoli manne akifuatiwa na Felix Sunzu mwenye magoli matatu, lakini hii leo atokuwemo katika kikosi kitakacho wavaa Mtibwa kutokana na majeraha aliyo nayo.

Wachezaji wengine wasimba wanaotarajiwa kukosa mchezo waleo ni pamoja na Amir Maftah aliyeumia katika mchezo zidi ya Kagera Sugar, pamoja na Salum Machaku na Mwinyi Kazimoto anaye tarajiwa kurejea uwanjani wakati wowote hivi sasa.

Simba wamesema hawapo teyari kupoteza point kama walivyo fanya katika michezo mitatu iliyopita.

Mtibwa Sugar ambayo kila msimu huondokewa na nyota waliongara na kuwapa wengine nafasi ya kuonyesha uwezo wao bila kuiyadhiri timu hiyo yenye maskani yake katika miwa ya Turiani.

Mtibwa Sugar ambayo iko nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi, silaha yao kubwa ipo kwa mtokea benchi Hussein Javu, akisaidiana vilivyo na nyota wengine akiwemo Salum Swedi mpya (mdogo wake Salum Swed anae kipiga Msumbiji na ametamba na uzi wa Mtibwa Sugar, Simba na Azam).

Mkongwe katika timu hiyo Shaban Nditi ataendelea kuongoza safu ya kiungo cha Mtibwa Sugar huku Vicent Barnabas akitarajiwa kutumika katika kupeleka mashambulizi kwa kasi langoni Mwasimba.

Mtibwa Sugar baada ya kutoa sare na Polisi Dodoma leo hawatakuwa na cha kupoteza na wanahitaji ushindi kuzidi kujikita katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo.


KAGERA SUGAR KUWAKARIBISHA POLISI DODOMA.


Mchezo mwingine wa ligi kuu utapigwa mkoani Kagera katika uwanja wa Kaitaba ambapo Kagera Sugar watawakaribisha Polisi Dodoma.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.