wachezaji

Soka: zengwe lanitoa Bongo


Mshambuliaji aliyeipandisha ligi kuu Mbagala Market (African lyon) Yusuph Soka ameibuka na kusema zengwe la soka la bongo ndilo limemfanya akimbie Bongo na klabu yake ya African Lyon.

Soka akiwa na umri mdogo na mshirika wa Mbwana Samatta katika klabu ya African lyon ameibuka baada ya kusemwa mengi juu yake, katika redio ya watu Clouds FM na kumwaga cheche zake kwa Lyon ambayo inaishutumu TFF juu ya utata wa wapi alipo.

Soka akizungumza na sports xtra ya Clouds FM alisema kuwa yeye hana wakala na hakuna mtu aliyempeleka Sweden na klabu ya AFC iliyo muita kwa ajili ya Majaribio alipata nafasi hiyo kupitia kwa Thomas Ulimwengu pale alipo ulizwa juu ya mchezaji mwenye umri chini ya miaka 20 anae mkubali Tanzania na kumtaja yeye.

Soka alienda mbali pale alipo sema Lyon walikuwa wameshaanza kumuundia Zengwe la kumtaka kumpoteza katika soka la bongo, hivyo mwanya huo ulipotokea, hakusita kuutumia kwa kujigharamia safari yake na malazi nchini Sweden ambapo bado yuko huko.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.