Leo azam fc walikuwa wenyeji wa Prisons na kufanikiwa kupata ushindi wa goli 3-0, wakati simba sc wakikubali kufungwa na Kagera sugar goli 1-0, katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya vodacom.
SIMBA WAVUNA POINT 1 KWA WAKATA MIWA.
Simba sc wamefanikiwa kupata pointi 1 kati ya 12 toka kwa wakatamiwa wa Kageqa sugar na mtibwa sugar baada ya mchezo wa leo uliochezwa katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.
Katika mchezo wa leo Kagera sugar wamepata ushindi wa goli 1-0, goli lililofungwa na Amandus Nesta kathka dakika ya 46 kabla ya Kagera sugar kupata pigo katika dakika ya 87 kufuatia mchezaji wao kupewa kadi nyekundu.
AZAM WATOA KIJOTI CHAMANZI
Kipre Tchetche leo ameongoza zoezi la utoaji wa kijoti kwa Prinsons katika nyasi bandia za azam complex zilizopo Chamanzi.
Kipre Tchetche amefunga magoli mawili katika dakika ya 18 na 85 katika ushindi wa azam fc wa goli 3-0 mbele ya Prisons wakati goli jingine likifungwa na John Bocco.
KAGERA SUGAR WAMFIKIA SIMBA
Kagera sugar wamefikisha point 34 ambazo ni sawa na point 34 za Simba sc wakitofautiana katika uwiano wa magoli ya kushinda na kufunga.
Azam fc wao wamefikisha point 40 wakiwa nyuma kwa point 8 toka kwa vinara yanga wenye point 48
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION (Tunarejesha uhai wa computer)
www.aboodmsuni21.blogspot.com/p/msuni-computer-solution_7934.html
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION (Tunarejesha uhai wa computer)
www.aboodmsuni21.blogspot.com/p/msuni-computer-solution_7934.html
0 comments:
Post a Comment