yanga

Maximo kutua Bongo Jumapili


Marcio Maximo

Kocha wazamani wa timu ya taifa 'Taifa Stars' Mbrazil, Marcio Maximo anataraji kutua nchini kwa mara nyingine tena toka aondoke nchini mwezi juni mwaka 2010 siku ya jumapili juni 17 saa 9 alasiri.

Maximo anakuja nchini kuchukua mikoba ya Mserbia wa Yanga Kostadin Papic aliyenyimwa mkataba, baada ya ule wa awali wa miezi 6 kwisha wakati ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/12 ukielekea mwishoni.

Maximo awali alitarajiwa awasili nchini hapo kesho, na kwa mujibu wa taarifa zilizo naswa na Sports In Bongo zinasema kocha huyo mwenye msimamo mkali atawasili jumapili na shirika la ndege ya Emirates.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa kocha huyo aliyekuwa amewafungia mlango kipa namba moja nchini Juma Kaseja, na Viungo Athuman Iddi Chuji pamoja na Haruna Moshi Boban, safari yake imesogezwa mbele baada ya kuobwa na klabu aliyokuwa anaitumikia kuwaandalia program ya maendeleo.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.