Ushapata kujiuuliza kwanini mchezaji bora wa mwaka kwa klabu ya Azam FC John Raphael Bocco 'Adbayor' kuwa mchezaji anaeongoza kwa kuzomewa hapa nchini pale anapo onekana kiwanjani bila ya hata kuugusa mpira.
Mfumania nyavu huyo wa Azam FC anaevalia uzi namba 19 akiwa amecheza michezo 62 ya ligi kuu ya vodacom ameziona nyavu za wapinzani wake mara 53 na kushikilia rikodi ya ukinara wa magoli ndani ya klabu yake ya Azam FC, ambayo ndiyo iliyo muibua toka Kijitonyama FC ya jijini Dar es salaam.
Pamoja na kuziona nyavu mara kwa mara akiwa na uzi wa Azam FC, mambo yamekuwa magumu akiwa na uzi wa Taifa Stars ambapo kuonekana kwake kwenye maandalizi ya mwisho (warming up) kabla ya mchezo teyari mashabiki wameshaanza kumzomea.
Kutokana na mashabiki wa mpira nchini kugawanyika katika makundi mawili ambayo ni Simba na Yanga, na ndie mchezaji katika kizazi hiki na huenda ni katika historia ya soka la Tanzania kufunga magoli mengi katika mechi zidi ya Simba na Yanga, akiwa amefunga magoli 23 katika michezo 28 dhidi ya timu hizo.
John Bocco ndie Mtanzania aliye ziona nyavu za Juma Kaseja, ambaye anaaminika kuwa Tanzania One kwa kipindi cha miaka 10, mara nyingi zaidi, akiwa ameziona mara 14, ambayo ndio magoli ambayo Bocco ameifunga Simba SC katika michezo 15 aliyocheza.
Chaguo la kwanza la yanga golini Yarm Berko kafungwa magoli 5 na Bocco kati ya 9 aliyoifunga yanga katika michezo 13 aliyocheza dhidi ya Yanga.
Akiwa na miaka 23, John Bocco akicheza kwa mara ya kwanza michuano ya Kagame Cup akiwa na timu yake ya Azam FC ameshaona nyavu mara 4, akiwa nyuma Taddy wa AS Vita mwenye magoli 6 na Said Bahamuzi wa Yanga mwenye goli 5, huku akiwa na taji moja la Kombe la Mapinduzi na kutwa ufungaji bora katika mashindano mawili ambayo ni ya Kombe la Mapinduzi na Ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/12.
0 comments:
Post a Comment