CECAFA

Manji amfunika Bakhalesa

Mfanyabiashara na Mwenyeketi wa Yanga Yusuph Manji amemgalagaza mfanyabiashara mwenzake Bakharesa, kufuatia magoli mawili yaliyofungwa na Hamisi Kiiza na Said Bahamuzi katika mchezo wa fainali ya kombe la Kagame.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Taifa, vijana wa Bakharesa 'Azam FC' waliuwanza mchezo kwa kasi na kupoteza nafasi kadhaa huku vijana wa Manji 'Yanga' wakipeleka mashambulizi ya kushtukiza.

Katika mchezo huo kipindi cha kwanza kulikuwa na kila aina ya ufundi, toka pande zote mbili, huku Azam FC wakitawala kipindi hicho chote.

Dakika ya 44 nahodha wa Azam FC Aggrey Morise alirejesha mpira nyuma taratibu ulionaswa na Hamisi Kiiza na bila ajizi Kiiza alimchambua Deo Munich 'Dida' na kuipeleka Yanga mapumziko wakiwa wanaongoza goli 1-0.

Azam walirejea kipindi cha pili kwa kuendelea kutawala mchezo, huku wakicheza muda mrefu katika lango la Yanga bila mafanikio.

Yanga walionekana kuwa na madhara pale wanapokuwa na mpira na katika dakika ya 92 Said Bahamuzi kufunga goli la pili na mpira kwisha kwa Azam FC kulala goli 2-0.

Kwa matokeo hayo Yanga wamefanikiwa kutetea ubingwa wa Kagame huku AS Vita wakiibuka mshindi wa tatu baada ya kumchapa APR goli 2-1 katika mchezo wa awali.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.