simba

Twite azidi kuwaumiza Simba, amwaga wino Jangwani

Dirisha hili la usajili linalo tarajiwa kufungwa jumatano hii limekuwa baya kwa Simba SC, baada ya kuchukuliwa beki yao wanao dai alikuwa na mkataba nao Kelvin Yondani na wapinzani wao wa jadi Yanga, kisha Ibrahim Rajabu Jeba wakadai wamemsajili na kuonekana katika mazoezi ya timu yao kabla ya kurejea katika timu aliyokuwa na mkataba nayo Azam FC.

Wakiwa hawajui nini hatima ya kiungo waliomsajili Ramadhan Chombo 'Redondo' anaedaiwa kuwa na mkataba na Azam FC, hivyo Azam FC kumjumuisha katika usajili wao. Mambo yamekwenda kombo jijini Kigali baada ya Twite kuwapiga changa la macho na kumwaga wino kwa Yanga.

Klabu ya Simba leo imeamua kutoa hadharani mkataba wake uliosaniwa  baina yao - klabu na mchezaji wa kimataifa kutoka Rwanda Mbuyi Twite ambaye muda mchache uliopita amesaini mkataba mwingine wa kujiunga na Yanga.

Kusoma vizuri jaribu ku-double click then maandish yatasomeka kwa ukubwa






Picha za mkataba ni kwa msaada wablog ya Shaffih Dauda


Na Kutoka Katika Mtandao wa Yanga

Mlinzi wa kati wa timu ya APR kutoka nchini Rwanda Mbuyu Twite amekalisha usajili wake ikiwa ni pamoja na kupata uhamisho wa kimataifa ITC na kuweza kujiunga na mabingwa wa kombe la klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kombe la Kagame timu ya Young Africans Sports Club.

Mbuyu Twite amabye zoezi lake la usajili lilianza takribani wiki mbili zilizopita limefikia mwisho baada ya klabu ya Young Africans kufanikiwa kupata uhamisho wake wa kimataifa kutoka timu aliyokuwa akiichezea ya APR ambapo awali alikuwa akiichezea timu ya Lumpopo st.

Twite ambaye alingara sana katika mashindano ya Kagame yaliyomalizika hivi karibuni na Young Africans kuibuka mabingwa, amesema anajisikia furaha na mwenye bahati kufanikiwa kujiunga na mabingwa mara mbili mfululizo wa kombe la Kagame.

Usajili wa Twite ulianza takribani wiki mbili zilizopita ambapo mjumbe wa kamati ya Utendaji wa klabu ya Young Africans Abdallah Bin Kleb aliamua kwenda nchini Rwanda kuhakiksiha zoezi hilo linakamilika haraka ipasavyo, ambapo mara baada ya kumalizana na Twite aliendelea kuhakikisha anafuatilia ITC yake.

Akiongea na www.youngafricans.co.tz Bin Kleb amesema, Young Africans ni timu kubwa katika Ukanda huu, Viongozi wake wanafanya mambo yao kwa uhakika zaidi, hivyo hawakutaka kuongelea suala la Twite mpaka watakapoona wamekamilisha zoezi lote'

"Unajua usajili sio mchezaji kusajuli makaratasi ya mkataba tu, kuna kupata barua ya kumruhusu kutoka timu anayotoka, uhamisho wa mchezaji kutoka chama husika cha soka cha nchi, baada ya hapo ndio unaweza kutangaza sasa kwamba ni mchezaji wako halali"alisema Bin Kleb.

Kusajiliwa kwa Mbuyu Twite kunaifanya timu ya Young Africans kuwa na ukuta wa walinzi wa kimataifa akiwemo Kelvin Yondani, Nadir Haroub Cannavaro, Ladislau Mbogo na Ibrahim Job kwa nafasi ya ulinzi wa katikati.

Twite anatarajiwa kuwasili mapema wikii kuungana na wacheji wenzake katika mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara inayotarajiwa kuaanza sepetemba mosi.
 

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.