ZGPL

JAMHURI NA BANDARI WATOA VICHAPO ZGPL

Na Ally Mohammed, Zanzibar

 Ligi Kuu ya Zanzibar, maarufu Zanzibar Grand Malt Premier League (ZGPL) iliendelea tena hapo jana kwa michezo miwili, katika uwanja wa Amaan mjini Unguja, Malindi ambao wamenunua daraja kutoka kwa timu ya Miembeni SC, waliteremka uwanjani kuivaa Bandari ambayo imepanda daraja msimu huu.

Katika mechi hiyo Bandari wameianza vyema ligi hiyo baada ya kuchomoza na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Malindi mabao ya Bandari yakifungwa na Mussa Omar katika dakika ya 31 kipindi cha kwanza bao la pili likifungwa na Haisam Khamis dakika ya 57.

Huku bao la 3 likfungwa na Shariff Kitwana katika dakika ya 78, na mabao ya Malindi yakifungwa na Amour Suleiman katika dakika ya 44 na 68.

Wakati katika kisiwa cha Pemba wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya kombe la shirikisho, Jamhuri wakicheza na Duma ambayo inamilikiwa na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) wameanza vizuri baada ya kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0, mabao ya Jamhuri yote mawili yakifungwa na Mfaume Shaaban katika kila kipindi, bao la kwanza akilifunga katika dakika ya 7 ya kipindi cha kwanza, bao la pili akifunga katika dakika ya 72.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.