AZAM KUANZA SAFARI YA KILELENI KESHO KOMBE LA SHIRIKISHO

Mabingwa mara mbili mfululizo wa kombe la mapinduzi Azam fc kesho itakuwa inaandika historia mpya ya kucheza kwa mara ya kwanza michuano ya kombe la shirikisho la mpira wa miguu Africa CAF, pale watakapo wakaribisha wageni wengine wa michuano hiyo toka Sudan kusini timu ya Al-Nasri Juba katika uwanja wa taifa.

Azam ikiwa na kikosi chake kamili ukiwaondoa Waziri Salum na Samih Hajji Nuhu walio majeruhi wengine wote wako fiti kwa mchezo huo wa kwanza kwa azam katika kombe la shirikisho.

Wachezaji wa azam fc wakizungumzia mchezo huo kwa nyakati tofauti wameelezea zamira yao ya kuanza michuano hiyo kwa kasi kwa kuwafunga Al-Nasri Juba.

Kocha wa azam fc Stewart Hall atakuwa na mtihani wa kuamua kuendelea kutumia safu ile ile ya ushambuliaji iliyofunga magoli 8 katika michezo mitatu iliyopita ambayo inaundwa na Brian Umony, Abdi Kassim na Khamisi Mcha huku Kipre Tchetche akitokea benchi katika mchezo wa tatu na kufunga goli 2.

Ama kubadilisha safu hiyo ya ushambuliai kwa kuwaingiza wafungaji wa azam fc John Bocco na Kipre Tchetche, huku safu ya ulinzi na kiungo kutarajia kubaki vile vile kama ilivyo kuwa inaonekana katika michezo ya ligi kuu.

Azam fc wamekuwa wakifanya vyema katika makombe wanayoshiriki kwa mara ya kwanza huku wakiwa na rikodi mbaya ya kuanza kwa sare katika michezo yao ya awali katika makombe hayo.

--
MSUNI COMPUTER SOLUTION NDIO SULUHISHO LA COMPUTER YAKO
call us: +255-657-184-421
www.aboodmsuni21.blogspot.com

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.